Announcements

TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO 2018/2019

Posted On: 23rd May, 2018

NAFASI ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA TEKNOLOJIA YA VIWANDA VYA MISITU KWA MWAKA WA MASOMO 2018/2019

Mkuu wa Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) - Moshi anatangaza nafasi za kujiunga na mafunzo ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu kwa mwaka wa masomo 2018/2019.

A. Mafunzo yanayotangazwa

(i) Astashahada (Cheti) ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu (NTA - Level 4 & 5)

(ii) Stashahada (Diploma) ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu (NTA - Level 6)

B. Sifa za mwombaji

(i) MAOMBI YA ASTASHAHADA (CHETI): Awe amemaliza kidato cha nne na awe amefaulu kwa alama D katika masomo MANNE. Mawili kati ya hayo yawe aidha Biolojia, Kemia, Fizikia au Jiografia na mawili yawe ni masomo mengine yasiyo ya dini. Pia ufaulu wa Hisabati au Kiingereza utapewa kipaumbele.

(ii) MAOMBI YA STASHAHADA (DIPLOMA): Awe amemaliza kidato cha sita na awe amesoma michepuo ya sayansi na kufaulu angalau kwa principle moja au subsidiary mbili, au awe na astashahada (cheti) katika fani ya viwanda vya misitu au fani inayofanana na hiyo na ufaulu usiopungua 2.5 GPA

C. Ada

Ada ya mafunzokwa mwaka ni Tshs. 800,000/= tu.

Wanafunzi wote wanajitegemea chakula na malazi wawapo chuoni, hata hivyo chuo kina nafasi chache za hostel ambapo kila mwanafunzi atakayepata nafasi hiyo atalipia Tshs. 270,000 kwa mwaka tu.

D. Jinsi ya kutuma maombi

(i) Mwombaji atatakiwa kujaza fomu ya maombi ambayo atailipia Tshs. 10,000/=

(ii) Maombi yote yaambatanishwe na vivuli vya vyeti halisi (form four leaving certificate, result slip/certificate, birth certificate) pamoja na nakala halisi ya slip ya benki

(iii) Fomu za maombi zinapatikana Chuo cha viwanda vya Misitu (FITI) – Moshi, kwenye Tovuti ya Chuo (www.fiti.ac.tz)

E. Tahadhari

Mwombaji yeyote ambaye hatazingatia taratibu au mahitaji yaliyotajwa hapo juu maombi yake hayatafikiriwa. Aidha mwombaji atakayewasilisha vyeti na hati nyingine za kughushi atachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 08 Septemba, 2018. Maombi ambayo hayatapokelewa tarehe iliyotajwa hayatafikiriwa.

Maombi yote yatumwe kwa: MKUU WA CHUO, CHUO CHA VIWANDA VYA MISITU (FITI), S. L. P. 1925, MOSHI.


IMETOLEWA NA: MKUU WA CHUO - FITI